Wafanyabiashara wanaouza dawa feki za kuuwa wadudu wa zao la Pamba nchini wametahadharishwa kuwa watachukuliwa hatua kali endapo watabainika kuendelea kufanya biashara hiyo.
Hayo yamesemwa mapema hii leo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina alipokuwa akizungmza na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba katika kata ya Mwabusalu Wilayani Meatu Mkoani Simiyu.
Amesema kuwa wapo wafayabiashara wanaodhoofisha wakulima wa zao la Pamba kwa kuwauzia madawa yasiyo na nguvu na kutoweza kufanya kazi katika zao la Pamba na kupelekea kufa kwa zao hilo.
Aidha, Mpina amewataka wakulima wa kijiji hicho kinacholima zao hilo la mfano na kutoa mbegu bora pekee ya pamba nchini kuacha kilimo cha mazoea na kutumia fursa hiyo kuangalia kwanza maeneo wanayoishi kutokana na faida itokanayo na biashara ya zao la pamba.
Sambamba na hilo Mpina amewataka wakulima hao kuzingatia suala la utunzaji wa mazingira kwa kuyaandaa mashamba yao kwa wakati huku wakizingatia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi wanayokabilina nayo.
-
Video: Waziri Mkuu atembelea kiwanda cha kampuni ya SBC Tanzania Ltd
-
Dk. Ndumbaro, Mgongolwa Wateuliwa TFF
-
Rais Magufuli amuapisha Benedict Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi
Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano toka iingie madarakani imepandisha bei ya zao la pamba kutoka bei ya awali ya shilingi 600 kwa kilo mpaka mpaka sh. 1,200