Zaidi ya wavuvi 50 nchini Guinea wamelazwa hospitali kwa ugonjwa wa ngozi ambao haujatambulika, ikiwa ni siku moja baada ya mamlaka nchini humo kuanzisha uchunguzi wa tukio hilo.
Msemaji wa serikali, Ousmane Diallo amesema serikali tayari imeunda kamati yenye wawakilishi kutoka wizara za mazingira, uvuvi, afya, uchukuzi na madini ili kuweza kufuatilia ugonjwa huo.
Wavuvi katika harakati za kiuchumi. Picha ya Inc.magazine
Amesema, muonekano wa picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha dalili za ugonjwa huo kuwa ni nyuso za wavuvi kuvimba, huku midomo na mikono ikiwa na vipele na vidonda.
Hata hivyo, tayari kamati ya wanasayansi imechukua sampuli za maji ya bahari katika maeneo yanayoshukiwa, na sampuli hizo zinachunguzwa katika maabara za ndani na nje ya nchi.