Zikiwa zimebaki siku tatu kufikia Oktoba 25, hali ya kutotabirika haraka kirahisi kwa mgombea urais atakayeibuka mshindi katika uchaguzi wa mwaka huu imezua mengi ambapo mashabiki wenye uhakika na mgombea wao wameamua kuweka rehani vitu vyao vya thamani.

Watu hao wanaodaiwa kuwa wafuasi wa wagombea urais wanaoweza kuwekwa kwenye kundi la ‘die hard fans’, wameweka vitu kama magari, nyumba na hata wake zao wakiahidi kuwa endapo mgombea wao atashindwa wao watawapa wapinzani wao hivyo vitu ambavyo wanaandikishana.
 


 
Hivi karibuni, mkazi mmoja wa Mtaa wa Bendera ya CUF jijini Dar es Saalam, Martine Mkude ambaye ni mfuasi wa CCM amemuweka rehani mkewe akimuahidi mfuasi wa Chadema aliyekuwa anabishana naye, Juma Hassan kuwa endapo Edward Lowassa atashinda na kuwa rais wa Tanzania basi atampa mkewe amuoe kwa mara ya pili.

“Haki ya Mungu..! kama Lowassa akiwa Rais basi mimi nitakupa mke wangu umuoe upya,” alisema Juma Hassan katika ubishani uliomalizika baada ya kuandikishana ahadi hiyo kwa balozi wa nyumba kumi.

 

Mchezaji Wa Simba Akutwa Na Begi Uwanjani
Magufuli Aonya Wanaokimbilia Mahakamani Kuzuia Miradi