Kampuni za uwekezaji 13 kutoka Austria, zimefika  jijini Dodoma kwaajili ya kutafuta maeneo ya uwekezaji katika sekta za usafirishaji, elimu,kilimo, afya na ujenzi wa miundombinu

Akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na wawekezaji hao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Binilith Mahenge, amesema katika kikao hicho wamefanya mawasilisho kwa pande zote na jijilimeonyesha maeneo muhimu na fursa zilizopo.

Dkt. Mahenge alibainisha kuwa wawekezaji hao wameonyesha nia ya kuwekeza katika maeneo hayojambo ambalo ni muhimu kwa Mkoa wa Dodoma kwa kuwa ni makao makuu ya nchi

“Leo (jana) tumepokea ugeni mzito kutoka Austria wakitafuta maeneo ya uwekezaji.Tumepata muda wa kila mtu kuwasilisha kwa upande wake wenyewe wakituonyesha maeneowatakayowekeza na wenzetu jiji wakaonyesha fursa zilizopo pamoja na maeneo ya kuwekeza,”amesema Dkt. Mahenge.

Aidha Mahenge amesema miongoni mwa fursa nyingine wanazotafuta wawekezaji hao ni usafirishaji hasa wa treni zinazotumia nishati ya gesi na ni gharama nafuu ukilinganisha na usafiri wa sasa unaotumia mafuta ambayo sio rafiki kwa mazingira pia upatikanaji wa zao pekee la zabibu katika Mkoa wa Dodoma na bidhaa zakeni nzuri ikilinganishwa na zinazozalishwa katika maeneo mengine.

Waziri Mkuu ahimiza utafiti kilimo cha mboga na matunda
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 6, 2020

Comments

comments