Kocha Mkuu wa Coastal Union, Fikiri Elias, amethibitisha kuwakosa nyota wake wawili, Khatib Kombo na Gerald Gwalala, kwenye mchezo wao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kupigwa Juni 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Elias amesema: “Wachezaji wote waliokuwa majeruhi awali wamerejea katika hali yao ya kawaida na wanaendelea kujiwinda dhidi ya Azam, isipokuwa tutawakosa nyota wetu wawili ambao ni Khatib Kombo na Gerald Gwalala.

“Kombo ana matatizo ya kifamilia ambayo ameenda kuyasuluhisha lakini kwa upande wa Gwalala tutamkosa kwenye mechi takriban tatu kutokana na adhabu yake ya kadi.

“Tuna mechi ngumu sana mbele yetu, Azam ni wapinzani wakubwa sana lakini mechi hii wataicheza kwetu na siku zote mcheza kwao hutunzwa hivyo lazima tuhakikishe kuwa tunapata ushindi na sapoti ya kutosha kutoka kwa wadau na mashabiki wa Coastal Union.”

Makamba ataja maeno 14 usafirishaji, usambazaji wa Umeme
Wanawake Halmashauri 184 nchini wapokea zaidi ya Bilioni 30