Watu wawili wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha magari mawili, Toyota Costal zenya namba ya usajili T 916 BQT iliyokua inatokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro kugongana  na lori lenye namba za usajili T . 793 DAT.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa kumi na moja alfajiri  ya Machi 20, 2022 eneo la Nanenane Manispaa ya Morogoro Barabara ya Morogoro – Dar es salaam

Akithibitisha kupokea kwa miili hiyo muuguzi wa zamu hospitali ya Rufaa  mkoa Morogoro Joyce Kiwale anasema kati ya hao majeruhi 15 majeruhi 12 wametibiwa na kuruhusiwa huku 3 wakiendelea na matibabu.

Akizungumza na Dar24Media kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro (SACP) Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mororgoro linaendelea na operasheni mbalimbali za usalama barabarani lakini pia kutoa elimu kwa madereva ili kuepukana na ajali zinazosababishwa na uzembe wa dereva.

Aidha Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia Dereva wa Lori mkazi wa Moshi kwa mahojiano licha ya taarifa za awali kuonesha chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa coster ambaye ni marehemu kuendesha gari bila tahadhari.

Ajali hiyo imetokea ikiwa imepita siku mbili baada ajali nyingine kutokea  eneo la Melele Barabara ya Morogoro – Iringa na kuua watu 23.

Bwawa la Chamakweza kufanyiwa marekebisho
Dkt.Tulia: Rais Samia kawapunguzia mzigo wanawake