Watu wawili wamefariki Dunia katika matukio mawili tofauti kufuatia kutokea kwa ajali ya kugonga Treni Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro na miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio la kwanza limetokea majira ya saa 12 asubuhi eneo la Mabogini lililopo kata ya Bomambuzi ambapo mkazi wa eneo hilo Salim Abuu (25), alifariki kwa kuigonga treni wakati akivuka reli bila tahadhari akiwa amelewa.

Gari Moshi. Picha ya Saturday evening Post.

Amesema, katika tukio la pili lililotokea majira ya saa tano asubuhi eneo la Stesheni kata ya Kahe, wilaya ya Moshi, mzee wa umri kati ya miaka kati ya 75 hadi 80 mkazi wa Kahe ambaye bado hajafahamika aliyekuwa na tatizo la kutokusikia alifariki kwa kuigonga treni wakati akivuka.

Amesema, “Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linaendelea kusisitiza kwa wananchi waache tabia ya kutembea barabara ya treni bila kuchukua tahadhari, kufanya hivyo kunapelekea vifo vinavyoweza kuepukika na serikali kupoteza nguvu kazi ya Taifa letu.”

29 wafariki tukio la kumkamata mtoto wa El Chapo
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 7, 2023