Ndege ya Kampuni ya Coastal Aviation iliyobeba watalii 10 imeanguka na kujeruhi watalii wawili na rubani ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Lobo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Hayo yamesemwa hii leo na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema ambapo amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana Jumatano Oktoba 25,2017 saa tisa alasiri ilipokuwa ikitua.

Amesema kuwa taarifa za awali kuhusu chanzo cha ajali hiyo ni mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha ambapo ilisababisha uwanja kujaa maji. hivyo wakati rubani akitua ndipo ndege ilianguka na kusababisha watalii hao wawili kujeruhiwa.

“Waliojeruhiwa ni wawili na rubani ambao walipelekwa jijini Arusha na baadaye Nairobi kwa matibabu. Wengine walikuwa na maumivu kidogo ambao walipatiwa huduma na daktari wetu na baadaye wakasafirishwa kwenda Arusha,”amesema Mwakilema.

Aidha, Mhifadhi huyo amesema kuwa wakati ndege hiyo ikianguka mbele kulikuwa na mawe, hivyo ingeyagonga na kulipuka ingesababisha madhara makubwa.

Msando apata shavu serikalini
Madaraja jijini Dar yasombwa na maji