Serikali ya Iran imewanyonga wanaume wawili, Sadrollah Fazeli Zare na Youssef Mehrdad baada ya kukutwa na hatia ya kumtusi Mtume Mohammad na kuichoma Kurani.

Kulingana na mahakama hiyo ni kuwa Machi 2021, mmoja wa washtakiwa alikiri kuchapisha maudhui hayo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii.

Wawili hao pia walishutumiwa kwa kumiliki akaunti za mitandao ya kijamii na vikundi ambavyo vinaendeleza ukafiri na kudhalilisha dini ya Kiislamu ambapo shirika la Habari la Mizan lilisema Sadrollah Fazeli-Zare na Yousef Mehrad walinyongwa katika gereza la Arak lililopo katikati mwa Iran.

Ripoti ya pamoja ya Human Rights – IHR, na Together Against the Death Penalty – ECPM, inaeleza kuwa watu 582 walinyongwa nchini Iran mwaka 2022, idadi ambayo ni kubwa zaidi tangu mwaka 2015 na ni zaidi ya wa 333 walionyongwa mwaka 2021.

Kocha Ihefu FC: Tunazitaka alama tisa zilizosalia
Erik ten Hag apotezea ya De Gea