Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, ametoa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania – EJAT, kwa mwaka 2022.
Washindi wa Tuzo hizo ni Waandishi wawili Francis Kajubi wa The Guardian na Cosmas Mwamposa wa Pangani FM.

Aidha, Jumla ya tuzo saba za umahiri katika uandishi wa Habari nchini Tanzania – EJAT, zilienda kwa waandishi nyota wa Dar24 Media.
Tuzo hizo zinazoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania – MCT, zimetolewa jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mlimani City Julai 22, 2023.