Kamati ya utendaji ya Young Africans chini ya mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla imewateua Suma Mwaitenda na Haruna Batenga kuwa wajumbe wa kamati hiyo.
Uteuzi wa wawili hao, umekuja baada ya wajumbe Rogers Gumbo, Shija Richard na Said Kambi kutangaza kujiuzulu juma lililopita.
Mbali na kujiuzulu kwa wajumbe hao, pia kamati ya utendaji ya Young Africans iliwachukua hatua za kinidhamu wajumbe Salim Rupia na Frank Kamugisha.
Maamuzi ya kujiuzulu na wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu, yaliyotakana na sintofahamu iliyoibuka kati ya mdhamini wa klabu hiyo kongwe nchini Kampuni ya GMS na uongozi, kwa kusitisha baadhi ya huduma ambazo hazipo kwenye makubaliano ya kimkataba.