Gwiji wa soka wa England, Wayne Rooney, anaamini, Declan Rice atathibitisha ni mchezaji mkubwa na kiongozi muhimu kwa Arsenal, wakati wakijaribu kuwania taji la Ligi Kuu England katika msimu mpya.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 alikamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 105 kutoka West Ham hadi kutua kwenye Uwanja wa Emirates wikiendi iliyopita, akisaini mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo ya Kaskazini ya jiji la London.

Mara moja Rice aliondoka na wachezaji wenzake wapya hadi Washington DC, ambapo Arsenal walianza ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya huko Marekani dhidi ya nyota wa Ligi Kuu ya nchi hiyo (MLS), juzi na walishinda mabao 5-0.

Kocha Mkuu wa DC United, Rooney ndiye aliyekuwa akiwaongoza nyota wenyeji na anaamini vijana wa Mikel Arteta wamepata sifa muhimu wanapotazamia kushinda taji la Ligi Kuu England la msimu huu mpya.

“Nadhani anaweza kuwa ndiye vizuri, lazima awe anayeweza kiongozi sasa, kwa kweli, nadhani timu ya Arsenal ilikuwa inamhitaji mtu kama yeye,” alisema Rooney

“Nilimwona Frank Lampard akisema anahisi Declan anaweza kuwa nahodha wa Chelsea kwa miaka 10, ijayo ikiwa angeenda huko.

“Nadhani anaweza kufanya hivyo (kwa Arsenal) na anaonekana kuwa na tabia hiyo na ninaamini atakuwa mchezaji mkubwa wa Arsenal.”

Rooney anajua jambo moja au mawili kuhusu matarajio yake baada ya uhamisho wa fedha nyingi, kwani yeye alistawi baada ya kujiunga na Manchester United kutoka Everton mwaka 2004.

Rooney mwenye umri wa miaka 37 anatarajia hivyo hivyo kutoka kwa Rice na kiungo mwenzake wa kati wa England, Jude Bellingham, ambaye mwezi uliopita alikamilisha uhamisho wa kujiunga na Real Madrid kwa dau la awali la Pauni Milioni 88.5 na kupanda hadi kufikia Pauni Milioni 115.

Namungo, Singida FG kupasha Arusha
Kocha Dabo afafanua mechi ngumu Tunisia