Shule ya msingi St.Florence Academy iliyopo Mikocheni Jijini Dar es salaam yakumbwa na tuhuma nzito baada ya mmoja ya walimu wa shule hiyo anayetambulika kwa jina la Ayoub Mlugu kusadikika kulawiti watoto wanne wa darasa la saba na mwalimu anayetuhumiwa kutoroka.

Hata hivyo baadhi ya wazazi wenye watoto katika shule hiyo tayari wameanza utaratibu wa kuwahamisha watoto wao baada ya taarifa hiyo mbaya kusambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari.

Baadhi ya wazazi waliopata nafasi ya kuongea na vyombo vya habari wamesema kitendo hicho kimewatisha sana na kusababisha hofu kubwa ya usalama wa watoto hao.

”Tulipopata taarifa za kubakwa kwa baadhi ya wanafunzi tumeogopa sana mimi mwanangu yupo darasa la saba na kitendo kimefanywa kwa wanafunzi wa darasa la saba, nimeogopa, nimeamua kuchukua uhamisho niwapeleke shule nyingine” amesema mzazi mmoja.

Aidha wazazi wameitaka serikali ingilie kati suala hilo na kufanya uchunguzi wa kina ili kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wa matukio haya.

”Tumeshangaa kusikia mwalimu amekimbia wakati uongozi wa shule unajua suala hili wiki mbili zilizopita siwezi kumuacha mwanangu, namuhamisha”.

Hata hivyo diwani wa kata ya Mikocheni, Venus Kimei ametembelea shule hiyo ili kujua kinachoendelea mara baada ya kupokea taarifa hizo na kusema kuwa anasubiri kikao cha maofisa wa polisi na uongozi wa shule ili kuchukua hatua mbadala.

 

 

Wananchi waandamana kupinga ufisadi Kenya
Singida United yatambulisha silaha mpya