Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamishina Msaidizi wa Polisi. Allan Bukumbi amesema vitendo vya ukatili vinavyojitokeza katika jamii vinatokana na mmomonyoko wa maadili na usimamizi mbovu wa baadhi ya Wazazi na Walezi kutowaangalia watoto wao.

Kamanda Bukumbi ameyasema hayo wakati alikuwa akizungumzia suala la ulinzi na usalama katika Maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini 2023, ambayo yamekusanya Mikoa kumi inayopatikana katika Nyanda za juu Kusini.

Amesema, hata hivyo jitihada za Jeshi la Polisi Kwa kushirikiana na Wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama zinasaidia kupata Taarifa za wahalifu na uhalifu na wao kuzifanyia kazi na ili hali iendelee kuwa shwari, doria kama za magari, miguu pamoja na pikipiki zimeimarishwa katika maeneo mbalimbali.

Aidha, Kamanda Bukumbi pia amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi linalo jukumu la kuelimisha jamii na pale tukio linapotokea linachukua hatua za haraka na wahusika hukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kwamba wageni wanaoingia ni wengi hivyo wanawaelimisha watu wanaowapokea kutoa taarifa Polisi pale wanapoona viashiria vya uhalifu.

Mabadiliko: Polisi wawe mfano kwa jamii - Manyinyi
Bilioni 80 za REA kutekeleza miradi ya Umeme Kagera