Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Tabora, Jovith Kato amewataka wazazi kujenga tabia ya kuwakagua watoto wao wanapotoka shule hasa kwa wale ambao wanatumia usafiri wa bodaboda na bajaji kutokana na ongezeko kubwa la matukio ya ukatili ikiwemo kulawitiwa.
Kato ameyasema hayo, wakati wa kutoa elimu kwa umma katika wiki ya sheria, amezungumza na walimu wote wa manispaa ya Tabora huku lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya ukatili wa watoto, ambao wanafanyiwa wakati wa kwenda shule ama wakiwa wanareje nyumbani.
Amesema, ”Ukatili wa kijinsia umezidi katika jamii yetu watoto tunawapakiza kwenye bajaji, bodaboda wanalawitia wazazi inabidi tuwe makini na watoto na iwe somo kwa wananchi, usimpe mtoto wako bodaboda au bajaji ambaye humuamini na wakati mwingine jitahidi kumuogesha akitoka shuleni ili uweze kubaini yaliyotokea huko njiani.”
Nao baadhi ya Walimu wamesema, ”kuna watoto ambao wanaenda uani wawili watatu, inabidi uafuatili kwasababu inawezekana kuna vitu vingine vinaendelea wao kwa wao kwahiyo ni jambo ambalo kweli lipo na sisi kaam wazazi au walimu inabidi tulifanyie mkazo kwasababu jamii sasa hivi imeanza kubadilika”
”Inatakiwa kama wazazi tusiaamini sana dereva bajaji na bodaboda tuwalinde watoto wetu wakiwa wanaenda shule au wanaenda sehemu yoyote tuwawekee ulinzi na mara nyingi tuwe nao karibu pia” wamesema Walimu hao.