Wazazi wametahadharishwa kuwa makini na katika matumizi ya mitandao ili kuepuka changamoto za kuwasiliana na watu wasiofaa wakiwemo wahalifu wa mitandao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Elimu na Uhamasishaji kutoka TCRA – CCC Hilary Tesha, akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema wazazi wanapaswa kuchukua tahadhari nne muhimu na kutoruhusu matumizi ya mitandao kwa watoto.

“Kwenye mitandao kuna wahalifu ambao wanatumia njia za ulaghai kuwashawishi watoto kutoa taarifa nyeti kuhusu wao wenyewe au wazazi wao.”Amesema.

Malisa akata mzizi wa fitna kero za Wananchi

Ameongeza kuwa, katika mitandao ya kijamii kuna wanyanyasaji wa mitandaoni ‘Cyber Bullies’ ambao mara nyingi huwa na malengo ya kuwanyanyasa watoto kisaikolojia na kuwasababishia hofu au msongo wa mawazo.

Tesha amesema “Mafataki wa mtandaoni ‘Online Sexual Predators’ ambao lengo lao ni kuwarubuni watoto kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, kukumbana na maudhui yasiyofaa kama vile maudhui ya ngono na picha za utupu, matukio ya kihalifu na biashara haramu na habari potofu.

“Kupakua programu hatarishi au virusi vya kompyuta kupitia tovuti hatarishi, kubofya viunganishi hatarishi na pia kufungua viambatanisho vya barua pepe vyenye virusi vya kompyuta na hivyo kusababisha uharibifu wa taarifa na vifaa vya kielektroniki.”Amesema.

Tesha, amesema pia changamoto nyingine ni watoto kuingia kwenye matumizi ya simu kupindukia kutokana na fursa zinazopatikana mitandaoni kama vile michezo ya kompyuta, mitandao ya kijamii, katuni na muziki huwavutia sana watoto ambao baada ya muda huwafanya kuwa watumwa wa mitandao.

Aidha, amewataka wazazi kuwalinda watoto kwa kuwahamasisha kutumia mitandao ili umsaidie kwenye masomo yake kitaaluma zaidi na si vinginevyo.

“Mzazi ajifunze mitandao kwa upana wake kutamsiadia kuelewa athari, lakini pia kumsaidia kuzungumza na watoto wako, kuweka mipaka ya mambo ambayo mtoto anaweza na ambayo hawezi kuyafanya mtandaoni.”Amesema

“Ni muhimu kuweka masharti kwa mtoto ili ajue mipaka yake pindi awapo mtandaoni na sio kusubiri hadi kitu kibaya kitokee kwake”.

Manchester Utd yalengeshwa kwa Thomas Partey
Feisal Salum afurahia mapokezi Azam FC