Mkoani Lindi, wilaya ya Ruangwa wazazi wamekuwa chanzo kikubwa cha kuongeza idadi ya wanafunzi wa darasa la saba kufeli kwa wingi.

Hii ni kutokana na tabia ya baadhi ya wazazi kuwalazimisha watoto wao kuandika madudu katika mitihani yao ya darasa la saba ili wafeli wasiendelee na masomo ya sekondari badala yake kuolewa.

Tabia hiyo imekuwa ikifanywa sana na wazazi hao ambao wamejikuta hawana pesa ya kuwaendeleza watoto wao kusoma elimu ya sekondari matokeo yake huwataka waanze kujihusisha na mahusiano wakiwa bado wadogo na kuwafelisha katika mitihani yao huku wengine kuwatuma kutafuta baadhi ya mahitaji ya nyumbani ikiwemo mboga

Hayo yamebainishwa katika mdahalo ulioandaliwa na chama cha wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA)  wakati wakiendesha mdahalo wa wanafunzi kuhusu mila na desturi zinazochochea mimba za utotoni.

Ambapo wanafunzi hao walisema baadhi ya wazazi huwalazimisha kukataa shule au kuwashauri wakosee majibu ya mitihani ya darasa la saba ili iwe rahisi kwao kuolewa.

‘’Kuna mwenzetu mmoja alikuwa na akili sana, matokeo yalivyotoka hakufaulu kujiunga na sekondari tulipomuuliza alisema mama yake alimwambia aandike 0000 ili afeli aolewe’’ alisema mwanafunzi mmoja.

Hata hivyo Mratibu wa Elimu Kata, Nambilanje Lista Mziwanda amesema tabia ya wazazi kuwalazimisha wanafunzi kuandika madudu ni tatizo la muda mrefu lisilo na takwimu rasmi.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilu ametoa amri ya kuwachukulia hatua wazazi wanaoruhusu na kushawishi watoto kujifelisha wakiogopa majukumu ya kuwahudumia ukizingatia serikali ya awamu ya ntano inatoa elimu bure ngazi ya msingi na sekondari.

 

Sheria kali zatungwa kudhibiti maadili ya wasanii Uganda
Mahakama yaisajili kesi ya Zitto, CAG ahojiwa na Kamati ya Bunge

Comments

comments