Wazee wa Chama cha ACT- Wazalendo  Mkoani Kigoma wakiwakilishwa na Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee ya Chama hicho, Alhaj Jaffar Kasisiko wamesikitishwa na kauli aliyotoa Spika Ndugai kuwa anaweza kumzuia Zitto Kabwe asiongee chochote mpaka ubunge wake utakapokwisha

Katika taarifa iliyotolewa na Wazee hao imesema kuwa kitendo cha Spika kumzuia Zitto Kabwe kuongea bungeni ni sawa na kuwazuia wao wasiongee na shida zao zisiweze kutatuliwa.

“Inaonekana kauli hiyo imeshafanyiwa kazi na kitendo cha kumwita Zitto kwenye Kamati ni sawa na kupoteza muda, jambo hilo halimtendei haki kijana wetu Zitto Kabwe na sisi  wenyewe,”amesema Mzee Kasisiko.

Aidha wazee hao wamemtaka Spika Job Ndugai na viongozi wengine watazame mambo ambayo yanawaunganisha wananchi na viongozi kwa pamoja ili waweze kujiletea  maendeleo katika jamii.

Hata hivyo, Wazee hao wamesema kuwa wamesikitishwa na kitendo hicho kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwanyima haki wananchi waliomchagua Mbunge huyo.

Majaliwa aungana na JPM kumuombea Lissu
Video: Nas na Nick Minaji katika mahusianao?