Wazee wilayani Muleba Mkoani Kagera wamemuomba  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwawekea ulinzi kwa dhidi ya vijana wasio na maadili ambao wamekuwa tishio kwa maisha yao huku baadhi wakiwa ni jamaa zao .

Wazee hao wametoa kilio hicho wakati wakiongea na Dar24 Media ambapo wameeleza kuwepo kwa vitendo vya ukatili dhidi yao ambavyo wamekuwa wakifanyiwa na wale wanaotakiwa kuwa msaada kwao.

Wazee hao wameeleza kuwa vitendo ambavyo wamekuwa wakifanyiwa ni pamoja na kudhulumiwa mashamba, mali wanazomiliki, kupigwa na kufanyiwa vitendo vya ubakaji hali inayopelekea kuahatarisha maisha yao.

Umoja wa Mataifa kupitia idara yake ya masuala ya kiuchumi na kijamii, (UNDESA) umesema kuwa dhuluma dhidi ya wazee huathiri haki za kiafya na za kibinadamu za mamilioni ya wazee na hivyo suala hili lazima lipatiwe nafasi kimataifa.

Mwanasheria Teresia Bujiku ambaye ni Meneja wa shirika la MHOLA linaloshughulikia masuala ya msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto, amekiri kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji hasa kwa wazee ambapo ameeleza kuwa wamekuwa wakipokea kesi mbalimbali, nyingi zikihusu masuala ya mirathi na migogoro ya ardhi.

Bujiku amesema kuwa jamii imeondokana na masuala ya malezi na makuzi ya watoto hali inayopelekea kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili kwa vijana wengi, ambapo pia amewataka wazee wote nchini kuhakikisha wanaandika wosia kabla ya kufa ili kuweza kuondoa migogoro kwenye familia pale wanapofariki.

Baraza kuu  la Umoja wa Mataifa  lilitenga siku ya tarehe 15 mwezi Juni kila mwaka illi kupaza sauti za kupinga manyanyaso yanayowakuta wazee.

Mkutano wa NATO wamalizika, China, Urusi zakemewa
Zitto: Uteuzi wangu ni mpaka majadiliano