Baadhi ya wazee Nchini Kenya, ambao wamefikisha umri wa miaka 70 na wanaotakiwa kusajiliwa ili kupata msaada wa mahitaji mbalimbali, wamewataka Maofisa wa Usajili kuangalia nyuso zao kukadiria umri wao na si kutumia vitambulisho.

Wazee hao, wamesema wameamua kuyasema hayo baada ya kujitokeza sintofahamu ya watu wanaotengeneza Vitambulisho feki kuonesha wamezeeka, ili nao waweze kuingia katika mpango huo kama njia mojawapo ya kujikimu na ugumu wa maisha, uliolikumba Taifa la Kenya.

Wamesema, “hivi vitambulisho vitatudanganya, tunaomba hawa Maofisa watuangalie usoni halafu watukadirie iwapo tumefikisha hiyo miaka 70, watu wanakuja na vitambulisho feki havina uhalisia na umri wao kiuhalali sasa tushikwe kwa saa hii kupitia sura zetu.”

Usajili huo, unalenga kuinua jamii na kuwapatia wazee hao misaada ya chakula na kumudu matibabu kupitia mpango wa afya kwa jamii, huku wakiongeza kuwa wanahisi vitambulisho pekee haviashiri umri wao kamili, hivyo sura zitumike kama njia mbadala.

Sensa 2022: Makinda avipongeza Vyombo vya Habari
Uchumi: Serikali kujenga Kiwanda cha kubangua Korosho