Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka nchini (UDART) Suzana Chaula huku akiweka wazi kuwa tatizo lililopo kwenye miradi wa UDART si uwezo bali ni usimamzi mbovu.

Majaliwa amefikia uamuzi huo leo April 19, 2021 katika ziara yake alioifanya katika kituo cha UDART na kubaini utendaji kazi na ufuatiliaji mbovu katika ofisi hizo uliopelekea uwepo wa mabasi mabovu, mifumo ya kielektroniki na mrundikano wa tiketi katika vituo.

“Tunataka tujenge mradi awamu ya tatu kwenda Gongo la Mboto, tunajenga awamu hii kukusanya fedha kununua mabasi kwa ajili ya awamu nyingine uwezo huo upo, tatizo ni usimamizi hatuwezi kuvumilia msimamizi ambaye hawezi akiwemo na mkurugenzi wa fedha, hatuwezi vumilia utaratibu huu, hii fedha sisi tumekopa World Bank na tunalipa fedha yetu ya ndani ya walipa kodi wa Tanzania, leo tunaweka watu hawafanyi kazi vizuri,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Awali Waziri Mkuu ameeleza uwepo wa Mkurugenzi Mkuu UDART kwa miaka mitano katika mradi huo bila kuleta maendeleo yeyote ikiwemo ununuzi wa mabasi mapya huku baadhi ya watendaji wakifumbia macho ubadhirifu unaofanyika.

“Mtu anauza tiketi zake ndipoo auze za serikali na watendaji wapo, wanaona na hawachukui hatua, leo nimewauliza tangu Mkurugenzi Mkuu ameingia UDART ana miaka mitano amenunua mabasi mangapi?, hakuna hata moja anasema hana fedha,” waziri Mkuu Majaliwa.

Vifo vya Covid vyapindukia Milioni 3
Simba SC, Bocco kimeeleweka