Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Jama Hassan Khalif, nchini Somalia ameitaka mamlaka inayoratibu utoaji wa  huduma za intaneti nchini humo kuzima uwezo wa kufikia mitandao ya kijamii ya  TikTok, Telegram, na tovuti ya kamari ya 1xBet.

Waziri Khalif, ametoa gizo hilo katika taarifa yake huku akitaja sababu za kuzuia makampuni hayo kuwa ni usalama na kupambana na ugaidi na ukiukwaji wa mara kwa mara sheria wa makundi ya kigaidi yanayotumia mitandao ya kijamii huathiri usalama na utulivu wa jamii.

“Unaamriwa kuzima mitandao iliyotajwa hapo juu kufikia Alhamisi Agosti 24, 2023 saa kumi na moja jioni,” ilesema taarifa hiyo, yeyote ambaye hatafuata agizo hili atakabiliwa na hatua za kisheria zilizo wazi na zinazofaa,” aliongeza.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab mara kwa mara hutumia huduma ya kutuma ujumbe ya Telegram ili kuchapisha video zake, taarifa kwa vyombo vya habari, na sauti za mahojiano na makamanda wao na mara nyingi huchapisha habari kuhusu mashambulizi yake kwenye Telegram na tovuti nyinginezo.

Doumbia, Young Africans ngoma ngumu
Gift Fred afunguka kukaa benchi Young Africans