Waziri wa Nchi (OR-UTUMISHI), Jenista Mhagama ameshukuru Serikali kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo iliyopo Mkoani Ruvuma na kusema wanufaika wakubwa wa huduma za eneo hilo watakuwa ni wanawake, watoto na wazee.

Mhagama ameyasema hayo hii leo, Oktoba 18, 2022 wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Mkoani humo, na kuongeza kuwa Serikali itawapangia watumishi wa sekta ya afya ili waweze kufika kutoa huduma kwenye hospitali hiyo.

Waziri wa Nchi (OR-UTUMISHI), Jenista Mhagama. (wa pili kushoto).

Amesema, “Mwaka 2022/2023 Serikali itaajiri watumishi 30,000 kwenye ajira mpya, na wengi ni wa sekta ya afya na elimu, lengo ni kuhakikisha mahitaji muhimu katika jamii yanakuwa yanafanyika na kutolewa kwa ufanisi.”

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwasili Mkoani humo kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo, ambapo alitoa maelekezo kuwa mapungufu aliyoyaona katika baadhi ya miradi yafanyiwe kazi, ili kuleta maana halisi ya matumizi ya fedha za Serikali.

Nilitaka kusikia zito atasema nini: Rais Samia
Bei ya Mbolea kupungua, wakulima wafurahia