Waziri wa Wanawake nchini Nigeria, Aisha Alhassan amejiuzulu nafasi yake na kukihama chama tawala cha All People’s Congress.
Bi. Alhassan aliandika jana barua ya kujiuzulu na kueleza kuwa pamoja na mambo mengine, amesukumwa na tukio la chama hicho kumkatalia kugombea Ugavana katika jimbo la Taraba.
Anakuwa mjumbe wa pili wa baraza la mawaziri katika Serikali inayoongozwa na Rais Muhammadu Bushiri kujiuzulu ndani ya kipindi kifupi.
Wiki mbili zilizopita, Kemi Adeosun aliyekuwa mwangalizi wa masuala ya fedha alijiuzulu na kukihama chama hicho.
Hii ni mara ya kwanza kwa mawaziri kujiuzulu katika Serikali inayoongozwa na Buhari tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.
- Idadi ya waliokufa tetemeko Indonesia yazidi 80
- Video: Magufuli atoa siri ya kumtosa naibu waziri, Ya Lowassa kuwakumba vigogo CCM
Matukio ya hamahama hasa kwa wabunge nchini humo yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara, wengi wakikihama chama tawala. Mwaka 2019, nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi mkuu.