Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amemismamisha kazi Mhandisi wa Manispaa ya kinondoni Isack Mpaki leo Juni 20, 2021 mara baada ya kutembelea miradi mitatu katika halmashauri ya kinondoni ikiwemo mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi mwenge na kutorudhishwa na maendeleo ya mradi huo.

Waziri Ummy amefikia uamuzi huo mara baada ya kutembelea na kukagua miradi ambapo amesema hajaridhishwa na ujenzi wa miradi hiyo kwani tangu ilipoanza hadi sasa imefikia asilimia 46 ya utekelezaji wake, licha ya kuongezewa muda.

”Sijaridhishwa na hatua za ujenzi wa stendi ya mabasi Mwenge, zipo sarakasi kwenye huu mradi zipo sintofahamu kubwa ili niweze kujiridhisha nasimamaisha ujenzi na naunda timu ya kuchunguza miradi yote mitatu stendi ya Mwenge, uwanja wa mpira pamoja na jengo la utawala wa Manispaa ya Kinondoni nataka kujiridhisha,” amesema Waziri Ummy.

Aidha amemuagiza Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe kumletea timu huru siku ya jumanne, tarehe 22/06/2021 kwa ajili ya kuchunguza mikataba yote kuanzia mwanzo ili kujiridhisha.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 21, 2021
Kardinali Pengo atunukiwa cheti cha heshima na Makamu wa Rais