Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefanya mabadiliko kwa kuwaondoa watumishi sita katika nyadhifa zao kwa sababu mbalimbali za utendaji  uliosababisha kuzorota kwa   huduma ya maji Wilaya ya Newala na Nanyamba mkoani Mtwara.

Walioondolewa ni mhandisi Primy  Shirima (meneja wa Ruwasa mkoa), mhandisi Rejea Ng’ondya (mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi Mtwara-Mtuwasa), mkemia Alualus Mkula (mkuu wa maabara ya ubora wa maji mkoa), mhandisi Emanuel Konkomo (mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Makonde), mhandisi Renard Baseki (meneja wa Ruwasa- Newala) na Anza  Makala (mkuu wa kitengo cha manunuzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Makonde).

Imeelezwa kuwa wataalam hao wa sekta ya maji watapangiwa majukumu mengine na wizara.

Katika Hatua nyingine, waziri amemuelekeza katibu mkuu wa wizara hiyo kuharakisha mchakato wa kumpata mkandarasi ambaye atajenga mradi mpya wa Makonde.

Mradi huo hivi sasa miundombinu yake ya  imechakaa kutokana na kujengwa muda mrefu tangu miaka ya 1950.

Mapema Desemba, 2021, Aweso  alisaini kibali cha kuanza utekelezaji wa mradi mpya wa Makonde.

Lazima tukope : Rais Samia
Trillion 14.7 kujenga reli ya kisasa