Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza amemuagiza meneja wa wakala wa uchimbaji visima (DDCA),  Peter Mdalangwila kuhakikisha wanafika Mpwapwa Mei 29, 2021 kuchimba visima vitatu katika Wilaya hiyo ambapo ameagiza kimoja kichimbwe katika Shule ya Sekondari Berege ili kupunguza adha ya maji inayowakabili wanafunzi.

Ametoa kauli hiyo wakati wa  ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kilichopo halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.

Hata hivyo waziri Aweso ameagiza kuvunjwa kwa jumuiya ya maji katika kijiji cha Berege wilayani humo huku akitoa onyo la ubadhilifu wa fedha za jumuiya ya watumia maji katika mradi wa maji kwenye  kijiji hicho.

Waziri Aweso alipokea malalamiko ya wananchi kuhusu  jumuiya ya watumiaji maji kuwa fedha zinakusanywa lakini hazipelekwi benki.

Amemuagiza meneja wa Ruwasa Mpwapwa, Syprian Warioba kurejesha fedha zilizochukuliwa katika jumuiya ya watumia maji Berege kuwalipa wataalam kwa ajili ya usimamizi wa miradi kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Aidha ametoa wito nchi nzima kuwa kuanzia sasa Jumuiya zote za watumia maji nchini ziwe na mafundi sanifu wanaotoka chuo cha maji na kuwa na watu wenye sifa ya uhasibu na tayari wizara imeingia makubaliano na chuo hicho.

Simba yafunguka sababu ya Kagere kutocheza
Kiswahili kutumika mikutano ya AU