Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewapokea na kufanya mazungumzo na wajumbe kutoka nchini Brazil ambao wako katika ziara ya kwenda kutembelea Chuo cha  Michezo Malya Jijini Mwanza kwa ajili ya shughuli za kuendeleza michezo.

Wajumbe hao ambao ni Ndugu  Paulo Pan kutoka  International Promotion Through Sports  na Flavio Pazeto kutoka  Ubalozi wa Brazil nchini wamefika Jijini Dodoma Juni 23 2021

Katika mazungumzo hayo Mhe. Bashungwa amemshukuru Balozi wa Brazil nchini Mhe. Antonio Augusto Cesar na Serikali yao kwa kuitikia wito wa kikao cha Mei 21 2021 Jijini Dar es Salaam  kilichokuwa na ajenda ya kushirikiana katika sekta  maendeleo ya michezo nchini hasa katika upande wa soka na mchezo wa masubwi kwa kufanya Programu ya kubadilishana wakufunzi.

“Tumekubaliana kuanzisha ushirikiano na Paulo Pan kutoka International Promotion through Sports katika kuendeleza sekta ya michezo nchini” amesema Mhe.Bashungwa.

Makubaliano hayo ambayo Wizara  na International promotion Through Sports yatafikiwa  yatatoa fursa kujadili uwezekano wa  kukutana na Kamati ya Olimpik  ya Dunia na Shirika la UNESCO kuhusu  namna ya kutunisha Mfuko wa Maendeleo wa Michezo nchini.

Azam FC: Tunapendwa kila kona
Gomes afichua siri ya kumchezesha Chama