Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, ametoa onyo kwa wafanyabiasha watakaoficha sukari ili wapate faida kubwa bei inapopanda.
Waziri huyo ameandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa serikali itawashughulikia kikamilifu watakaobainika na njama za kuficha sukari.
Hata hivyo Bashungwa amesema Tume ya Ushindani (FCC,) na vyombo vya ulinzi na usalama wapo kazini kuchunguza.
Ambapo siku ya jana waziri Bashungwa aliwatoa hofu wananchi kuhusiana na sukari kupanda bei, alisema sukari iliyoagizwa kutoka nje ya nchi itaziba pengo la asilimia 20.
Hivi karibuni sukari imeanza kuwa adimu katika masoko huku gharama zake zikiwa hazishikiki kwa kuwa kilo moja imefikia sh 4,500 kutoka sh 2,500.