Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amewaagiza wakaguzi wa ndani katika Halmshauri zote kufanya kazi yao kikamilifu kwa kuhakikisha wanasimamia matumizi halisi ya fedha zinazotolewa na Serikali na wadau kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri zao.

Waziri Bashungwa ameyaeleza hayo wakati alipoambatana na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za mitaa kukagua ujenzi wa kituo cha afya Sagambi kinachojengwa kwa mapato ya ndani ya Halamshauri na nguvu za wananchi katika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

“Wakaguzi wa ndani simamieni miradi ya maendeleo na pazeni sauti pale mnapoona kuna hali isiyo ya kawaida kwenye matumizi ya fedha, wakaguzi wa ndani wakisimamia fedha inayotolewa na Serikali na wadau bila kumuonea mtu aibu tutaweza kuwafikishia huduma bora wananchi ndani muda mfupi” amesema Waziri Bashungwa

Waziri Bashungwa ameeleza kuwa anashangazwa na halmashauri ambazo kuna miradi iliyotekelezwa lakini haiendani na matumizi halisi utekelezaji wake na wakaguzi wa ndani wapo ila wanakaa kimya na kusubili Mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG) abaini mapungufu hayo.

Ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mbunifu kutafuta na kupata vyanzo vingi vya fedha zinazoletwa kwenye halmashauri kwahiyo lazima wawe wakali sana kuhakikisha kila fedha inaenda kufanya kazi yake kwa kila mradi katika Halmashauri na kusimamiwa kikamilifu.

Aidha, Waziri Bashungwa amepongeza wananchi na wadau wa Halmashauri ya wilaya Chunya kwa kuendelea kujitoa kwa hiari kuchangia miradi ya maendeleo ambayo inajengwa kwa fedha za ndani na amemuagiza Mkurugezi kuhakikisha fedha zote zinazotumika kunakuwa na uwazi na uwajibikaji katika matumizi yake.

Mradi wa Ujenzi wa kituo cha afya Sagambi unakadiriwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 500 ambazo ni fedha za mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya Chunya Mkoani Mbeya na mpaka

Diamond Plutnums alia na BASATA
Mulamula amtambua balozi wa Malawi Tanzania