Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa ametoa rai kwa wadau wa tasnia ya habari kuwa watulivu wakati huu serikali ikishughulikia madai ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusabilo Mwakabibi kuwaweka chini ya ulinzi waandishi wa habari.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Waziri Bashungwa ameandika, “Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunafuatilia malalamiko ya wadau ya tasnia ya habari juu ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusabilo Mwakabibi, kuweka chini ya ulinzi wanahabari. Tunaomba wanahabari wawe na subira wakati tunafanyia kazi suala hili.”

Mwakabibi anadaiwa kuagiza kukamatwa na kushikiliwa kwa waandishi wa habari wawili, Christopher James na Dickson Bilikwija kwa kuhudhuria Mkutano wake na wafanyabiashara wa soko la Mbagala kuu bila ya ruhusa yake.

Mkurugenzi huyo anadaiwa kutoa amri hiyo muda mfupi baada ya kuingia kwenye kikao hicho na kukuta waandishi hao wawili waliokuwa wamepewa mwaliko na wafanyabiashara hao, akidai hawakupaswa kuhudhuria.

Mtoto wa darasa la tatu afariki akiigiza watu wanavyojinyonga
Rais Mwinyi atumbua vigogo idara maalum