Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana leo April 4, 2022 amekutana na Wataalamu kutoka Idara ya Wanyamapori kwa lengo la kupata uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya Sekta ya Wanyamapori nchini .

Katika Kikao hicho Waziri Dkt.Pindi amewasisitiza watalaam hao kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu ili kuboresha Sekta hiyo kwa kuvutia Watalii na kuongeza Pato la Taifa hususani katika kipindi hiki ambacho tasnia ya utalii imeathiriwa na janga la UVIKO 19.


Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha pamoja na Wataalamu mbalimbali kutoka idara ya Wanyamapori.

Muhimbili yapewa miezi miwili kujitathmini kihuduma
Bunge la Tanzania kuanza kurushwa 'Live'