Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameziagiza kamati za Tiba na Dawa zilizobainika kuwa Mfu kutoa maelezo kwa mamlaka zao za ajira na kwa baraza la kitaaluma, huku akiwataka wafamasia kuimarisha kamati hizo katika ngazi zote kutokana na kwamba wao ndio makatibu wa kamati hizo.
Aidha Wafamasia nchini wametakiwa kufanya ajenda ya upatikanaji wa dawa iwe ya kudumu Kwenye kamati za ulinzi na usalama ngazi ya Kijiji, Kata,Wilaya na Mkoa.
Rai hiyo imetolewa leo Julai 30, 2021 na Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima wakati wa mafunzo ya usimamizi na Udhibiti wa bidhaa za afya kwa wafamasia wa Mikoa,Halmashauri na Hospitali uliofanyika jijini Dodoma.
Dkt. Gwajima amesema kuwa ajenda hiyo ikiwa endelevu Kwenye ngazi hizo Basi hakutakuwa na malalamiko ya upatikanaji wa dawa yanayoendelea kuwa hauridhishi
“Nitoe maagizo kwa viongozi wa ngazi zote ,wafamasia wa Mikoa,Halmashauri na Hospitali fanyeni ajenda ya upatikanaji wa dawa iwe ya kidumu Kwenye kamati za ulinzi na usalama ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya na Mkoa”, Amesema Dkt Gwajima.
Aidha, Waziri huyo amewaagiza wataalamu hao kwenda kusimamia Mwongozo wa Matibabu nchini na Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (STG/NEMLIT),kwani mwongozo huo toleo jipya la mwaka 2021 limezinduliwa.
Kwa upande wa matumizi ya Cheti Cha Dawa Dkt. Gwajima amewataka wafamasia hao Kwenye kusimamia Hilo Kama alivyoelekeza awali kanuni ya Cheti Cha dawa ‘The Pharmacy (Prescription Handling and Control Regulations, 2020) kwani imeandaliwa na imeanza kutumika.
Hata hivyo Dkt.Gwajima amewataka wafamasia hao kuhakikisha Kuna upatikanaji na matumizi sahihi ya nyezo muhimu za usimamizi wa bidhaa za afya zikiwemo leja ya Mali na hati ya kutoa na kupokea Mali,