Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amekagua shamba darasa la ng’ombe wa maziwa la kikundi cha UHAI katika Kijiji cha Mafai, ujenzi wa eneo la ukusanyaji maziwa, kisima, kikundi cha shamba la mfano la ufugaji nyuki pamoja na kilimo hifadhi cha zao la mahindi kwa kutumia teknolojia.

Ukaguzi huo umefanyika hii leo Mei 9, 2023 ambapo katika miradi hiyo, Dkt. Jafo amewapongeza kwa utekelezaji na kusema ameridhishwa kwani pamoja na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi inayoathiri kilimo mradi huo unasaidia wakulima kupata tija.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Khamis Mkanachi alisema miradi hiyo imeleta manufaa makubwa kwa wananchi wilayani humo hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na miradi hiyo hususan wa ng’ombe utaongeza thamani ya mifugo ambapo kupitia kilimo cha mahindi cha teknolojia ya kisasa inawasaidia wananchi kupata mazao na kukuza uchumi.

Mradi wa LDFS unaofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) unatekelezwa pia katika Halmashauri zingine ikiwemi Nzega (Tabora), Magu (Mwanza), Kondoa (Dodoma) na Micheweni (Kaskazini, Pemba).

Kiongozi Azam FC aingilia sakata la Fei Toto
Rais Samia azungumza na Diaspora wa Namibia