Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Selemani Jafo amekutana na Wadau wanaojihusisha na shughuli za kukusanya, kusafirisha, kuhifadhi, kuingiza nchini, kusafirisha nje ya nchi urejelezaji wa taka hatarishi ikiwemo taka za kielekitroniki ili kwa pamoja kuweza kujadiliana namna bora ya kukabiliana na changamoto.

Aidha amewataka wadau hao kutoa mapendekezo na maelekezo yatakayoimarisha usimamizi na udhibiti wa taka hatarishi nchini. 

Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na wadau serikali ilifanya mapitio na kufanya marekebisho ya Kanuni za Udhibiti wa Taka Hatarishi za Mwaka 2019 na kuandaa Kanuni mpya za Udhibiti na Usimamizi wa Taka Hatarishi za Mwaka, 2021 kufanya mapitio ya Kanuni za Ada na Tozo za Mwaka, 2019 na kuandaa Kanuni za Ada na Tozo za Mwaka, 2021.  

Akizungumza na wadau hao Waziri Jafo amesema kuwa lengo kuu la kufanya mapitio ya Kanuni lilikuwa ni  kuweka mfumo madhubuti wa usimamizi wa taka hatarishi nchini. 

“Ikiwa ni takriban miezi miwili sasa tangu Kanuni hizi zilipopitishwa mwezi Mei, 2021 na kuanza utekelezaji wake,  nimeona ni vyema pia tukumbushane matakwa ya Kanuni hizi na nyie wadau mtueleze changamoto mnazokumbana nazo katika kuzingatia matakwa ya Kanuni husika ili sote kwa pamoja tuweze kuimarisha usimamizi wa taka hizi,” Amesema Waziri Jafo.

Sambamba na hayo Waziri Jafo amewakumbusha Wadau hao  kuwa Tanzania imeridhia Mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda  ambayo inatoa fursa ya ushirikiano wa kimataifa katika kusimamia na kudhibiti usafirishaji wa taka hatarishi baina ya nchi na nchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Selemani Jafo akiongea wakati wa Mkutano na Wadau wanaosafirisha, kuingiza na kusambaza taka hatarishi katika ukumbi wa Millenium Tower jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kusikiliza changamoto za Wadau hao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Selemani Jafo akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati wa kikao hiko kilichokutanisha Wadau wanaosafirisha, kuingiza na kusambaza taka hatarishi.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Andrew Komba akiongea wakati wa Mkutano wa Wadau wanaosafirisha, kuingiza na kusambaza taka hatarishi katika ukumbi wa Millenium Tower jijini Dar es Salaam.

Wakurugenzi wote wa halmashauri za Unguja Nje
Adama Traore ahienyesha Liverpool