Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ameagiza kufanyika kwa marekebisho ya lambo lililochimbwa katika Kijiji cha Kazania Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma, ili liweze kuzalisha maji kwa kiwango kikubwa kama ilivyotarajiwa.

Jafo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika kijiji hicho kukagua lambo lililochimbwa kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mfumo Ikolojia Vijijini (EBARR), unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Amesema, “ofisi ya Makamu wa Rais imetoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii ya mazingira na tume hiyo ndio inaelekeza maeneo sahihi ambayo uchimbaji wa malambo unaweza kufanyika lakini hapa tume mmetuangusha nilitegemea katika mvua hizi lingekuwa limejaa na hapa naona wananchi wanachota maji yenye rangi hii ya udongo na yangekuwa meupe kama yangekuwa yamejaa kwenye lambo.“
 
Aidha, kutokana na hali hiyo Waziri Jafo amewaagiza wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
kufanya marekebisho ya lambo ikiwemo kutengeneza mifereji ifikapo Juni 2023 ili maji yaweze kupita kwa urahisi tofauti na ilivyo sasa.

Baleke ampa wazimu Moses Phiri, aahidi mazito Simba SC
Kipa Rivers United amtaja Mayele, Musonda