Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo ametoa siku 14 kwa Uongozi kwa Wilaya ya Kinondoni kuhakikisha wanatatua tatizo la mfumo wa majitaka katika Mtaa wa Ufipa, Dar es Salaam. 

Ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mtaa wa Ufipa na kujionea uharibifu mkubwa wa mazingira utokanao na mfumo wa maji taka ambao miundombinu yake imeharibika na kutiririsha maji taka katika makazi ya watu.

“Wataalamu msikae Ofisini tu, tokeni mje msikilize na kutatua kero za wananchi, haiwezekani mimi Waziri wa Mazingira nitoke Dodoma kuja kukagua na kuleta ufumbuzi wa tatizo hili wakati ninyi mpo hapa kila siku”amesema Jafo

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe amesema atahakikisha tatizo hilo linapatiwa ufufumbuzi ndani ya siku 14 kama Waziri Dkt. Selemani Jafo alivyoelekeza.

“Waziri nikuhakikishie, sisi Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi, siku ya Jumatatu yaani 28/02/2022 tutawasilisha kwako mpango kazi wa utekelezaji katika kutatua suala hili,” Gondwe alifafanua.

Watanzania takribani 300 kurejeshwa nchi wakitokea Ukraine
Grand P: Mimi na wewe 'dam dam'