Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amewaagizi Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote Nchini kuhakikisha wanadhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya ndani inayotokana na matumizi ya mifumo ya kielektroniki.

Ameyasema hayo wakati wa kufunga Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Pwani, Lindi, Mtwara na Arusha yanayoratibiwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi na kufanyika kwa siku Tano mjini Dodoma.

Amesema kuwa kuna baadhi ya Halmashauri ambazo mashine zake za Kielektroniki hazipeleki Fedha kwenye Akaunti ya Serikali na badala yake Fedha za makusanyo zimeelekezwa moja kwa moja kwenye akaunti za watu binafsi hili ni kosa kubwa sana Kisheria na linatakiwa kudhibitiwa haraka iwezekanvyo.

“Natoa mfano wa Halmashauri ya Kilindi ambayo mashine yake moja haiingizi Fedha kwenye Akaunti ya Serikali na badala yake fedha hizo zinaenda kwa watu wengine kabisa nakuagiza Mkurugenzi wa Kilindi kuwasilisha taarifa ya ununuzi wa mashine za Kielektroniki, mgawanyo wa mashine hizo kwa wahusika, matumizi yake, mchanganuo wa mapato yaliyopatikana kwenye halmashauri baada ya manunuzi ya mashine hizo na hatua ulizochukua baada ya kubaini kuwa mashine moja inapeleka Fedha Nje ya Mfumo,”amesema Jafo.

Hata hivyo, amezitaka Halmashauri zote Nchini, kuhakikisha viongozi wanafuatilia mashine za kieleketroniki kama zimeunganishwa kwenye Mfumo wa Serikali na hakuna hata senti moja inayopotea katika mazingira ya kutatanisha na pia maeneo mengine yote ambayo yanaweza kusababisha upotevu wa Fedha za  Serikali.

 

Live Ikulu: Rais Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa JWTZ
Wenger: Mpira wa miguu unaharibiwa na fedha