Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier na kufanya mazungumzo.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Kabudi amemueleza Mhe. Balozi Clavier kuwa, uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa ni wa muda mrefu ambapo hadi sasa Tanzania imekuwa na mahusiano imara na taifa hilo.
Hata hivyo pamoja na mambo mengine, mazungumzo yao yalijikita katika kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa, kuongeza ushirikino wa maendeleo, kuimarisha uwekezaji, biashara pamoja na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba wakati balozi huyo alipokutana na Mhe. Waziri leo