Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla amefanyiwa upasuaji wa kwanza katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu, Mgongo, Ubongo na Uti wa Mgongo Muhimbili (MOI), kutibu mkono wake ambao ulivunjika katika ajali aliyoipata Agosti 3, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi, ambapo amesema kuwa hali ya afya ya Dkt. Kigwangalla baada ya upasuaji huo inaendelea kuimarika.

“Madaktari wetu walimfanyia upasuaji Agosti 12, mwaka huu, hajambo, anaendelea vyema ni wito wetu kwa Watanzania kwamba waendelee kumwombea ili aweze kurejea katika majukumu yake ya kulitumikia taifa,” amesema Mvungi

Aidha, Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, amesema kuwa Dkt. Kigwangalla yupo anaendelea vizuri na matibabu.

Hata hivyo, Dkt. Kigwangalla amesema kuwa anamshukuru Mwenyezi Mungu kwani aliweza pia kufanya mazoezi hadi eneo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) ambako aliwahi kusoma.

 

Steven NZonzi kucheza Italia hadi 2022
Tabia mbaya usizozijua zinazozeesha katika umri mdogo