Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa leo Alhamis (April 08) anatarajiwa kukutana na uongozi wa Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ na klabu ya Young Africans kumaliza tofauti zilizopo baina ya pande hizo mbili.

Hayo yamesemwa Katibu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Dk Hassan Abbasi  jana Jumatano (April 07) kufuatia tetesi za Young Africans kutaka kufanya maandamano ya amani kupinga kile waanchoamini uonevu wa TFF dhidi yao.

“Nimesikia watu wanataka kuandamana sijui maeneo gani, hawa watu wa Young Africans wanaona kwamba kuna matatizo kwenye TFF au kuna msimamizi fulani, sasa hizi kelele zimekuwepo muda mrefu, kwa hiyo huwezi Serikali ukasema watu wanataka kuandamana iwe ni kweli, wametishia au hawapo halafu Serikali ukasema umetulia tu, kwa hiyo nafikiri hilo limekwishachukuliwa hatua,”

.”Kesho (Leo) mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo amewaita Young Africans kuwasikiliza kuna nini, lakini pia amewaita TFF wenyewe kwa upande mwingine nao kuwasikiliza kwamba kuna nini hiki, Kisha taratibu zile za kawaida za kimfumo wa mpira na taratibu hizo zitafuatwa,”

“Lakini kesho (Leo) hili ningeomba pia nilisistize kwamba kama kuna malalamiko yoyote, wadau watulie Serikali ipo, inasikiliza na vyombo vipo, yale yanayopaswa kubaki kwenye kanuni za michezo yatabaki, yanayohitaji mwongozo na maelekezo ya Serikali tutatoa, hivi ndivyo tunavyopaswa kwenda,” amesema Dk. Abassi.

KMC FC yatuma salamu Young Africans
Baraza, Kagera Sugar majaribuni Mbeya