Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeboresha miundombinu ili kuwavutia wawekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi na ajira.

Majaliwa ameyasema hayo wakati akitembelea maendeleo ya mradi wa machinjio ya kisasa ya Nguru Hills Ranch Ltd yaliyoko Mvomero Mkoa wa Morogoro.

“Tulipoanza huko tulikuwa tunaimarisha miundombinu na wapo watu hawakujua kwa nini tulianza na miundombinu. Miundombinu hii inarahishisha uwekezaji, tumejenga barabara, tumenunua ndege, tumeweza kujenga majengo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha uwekezaji pia kusambaza umeme maeneo yote,” amesema.

Machinjio hayo yanamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali kupitia Mfuko wa Pensheni wa PSSSF na Zubair Corporation kutoka Oman na Eclipse Investment LCC.

Waziri Ummy awasimamisha kazi viongozi wawili
Tetemeko la ardhi laua 304, maelfu wajeruhiwa