Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameitaka taasisi ya Shelter Afrique kuratibu maonesho ya kimataifa ya dunia ya Teknolojia na ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu nchini Tanzania.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo alipokutana na ujumbe wa taasisi hiyo katika ofisi za wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma uliokwenda kwa ajili ya kutangaza mikakati yake katika kusaidia ujenzi na teknolojia rahisi ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa nchi wanachama.

Lukuvi amesema, serikali iko tayari kutoa eneo kwa ajili ya kufanyika maonesho yatakayoshirikisha makampuni mbalimbali Duniani na kuongeza kuwa, maonesho hayo yataisaidia kutangazwa teknolojia za ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu.

‘’Tunataka Shelter Afrique mratibu maonesho na wadau wengine duniani kwa ajili ya kuonesha teknolojia mpya au teknolojia nyingine kwa ajili ya ujenzi wa nyumba bora na  gharama nafuu na maonesho hayo yawe ya kidunia,” Amesema Lukuvi.

Shelter Afrique ni Taasisi ya kifedha yenye nchi wanachama 44 Barani Afrika inayosaidia maendeleo ya ujenzi kwenye sekta ya nyumba  na maendeleo ya mijini nchini Afrika ambapo hutoa bidhaa na mikopo ya fedha kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba bora za makazi kwa gharama nafuu.

Bilioni 212.95 kununua ndege 5
Tanzania mwenyeji mkutano wa Utalii UNWTO