Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, amewataka Wakurugenzi wa halmashauri zenye masoko ya samaki ya kimataifa kuacha kupanga tozo za mazao ya uvuvi bila kuwasiliana na Wizara hiyo ili kuondoa kero za tozo zinazowakumba wananchi wanaofanya biashara katika maeneo hayo.
Mashimba ameyasema hayo baada ya kutembelea mnada wa mifugo uliopo Kijiji cha Buzirayombo, Kata ya Bukome na soko la samaki la kimataifa lililopo Kijiji cha Kasenda, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita ambapo Wizara haitaki kusikia kero za wafanyabiashara kuhusu tozo zisizo rafiki katika masoko hayo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chato Dkt. Medard Kalemani, amemuomba Waziri Ndaki kupitia vikundi vya wavuvi vilivyosajiliwa, Wizara ione namna ya kuwasaidia wavuvi mikopo yenye riba nafuu pamoja na kuwanunulia nyavu ili kuacha kujihusha na uvuvi usiofuata utaratibu.