Vyama vya Upinzani na Umoja wa Wanahabari wa Kenya, wamesema Waziri wa Biashara, Moses Kuria hafai kushikilia nyadhifa za umma kutokana na kitendo chake cha kuwatusi hadharani waandishi wa chombo kimoja cha Habari nchini humo.

Hatua hiyo, imefikiwa baada ya Waziri Kuria kukishambulia chombo cha habari cha National Media Group – NMG, na kuwatishia kuwafukuza kazi maafisa wa Serikali waliopeleka matangazo NMG.

Waziri Biashara wa Kenya, Moses Kuria.

Waziri huyo, Moses Kuria alijikuta katika mvutano huo pia na baadhi ya Viongozi Serikalini baada ya kuendeleza mfululizo wa matamshi yake ya dharau, dhidi ya chombo hicho na kuwatusi Wanahabari.

NMG kwa upande wake ilisema, Waziri Kuria anafanya yote hayo baada ya uchunguzi uliotangazwa na kituo chake, kuhusu kashfa zinazohusiana na mpango wa uagizaji bidhaa, unaoendeshwa na shirika la Serikali lililopo katika Wizara yake.

Mtihani ni lazima kabla ya usaili
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 22, 2023