Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mohamedi Mchengerwa ameishauri Jamii yote kutowanyanyapaa,kwa kuwabagua kuwaona wao si binadamu watoto wenye usonji kwani nao wana haki kama watoto wengine.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam katika mchezo mashindano wa mbio yaliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali Lukiza inauojishughulisha na watoto wenye usonji siku ikiwa na lengo la kuhamasiha jamii kuwa usonji siyo ugonjwa ni hali tu ya mapungufu ya ufahamu inayoweza ikamkumba mtoto au mtu mzima kwani binadamu kabla hajafa hajaumbika ni kauli inayosambaa kila mhali hivyo ni budi kutonyanyapaa watu wenye changamoto yoyote haijalishi mlemavu,mtu mwenye usonji.
“Niseme kuwa mtoto mwenye usonji ana haki ya kupata haki zote Kama watoto wengine ikiwemo huduma ya afya elimu ili kushirikishwa katika matukio ikiwemo michezo ili kumsaidia kujengeka vizuri kiafya na siyo kufungiwa ndani”amesema Waziri Mchengerwa.
Sanjari na hayo amesisitiza maafya michezo kusajili vikundi vyeote na kuvifuatili na kuvitambua ili kusaidia kunapotokea mashindano waende wakapeperushe bendera ya Tanzani
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojuhusisha na watoto wenye Usonji(Optism) Hilda Nkabe amesema wameandaa mashindano ya mbio jumuishi ambapo washiriki ni watu wa wote ikiwemo watoto ,wazee, vijana lengo likiwa ni kuelimisha jamii juu ya usonji ambapo mtu anakuwa hana tatizo lolote kimwili bali kiufahamu ndiyo ana tatizo hivyo jamii haina budi kunyanyapaa watoto hao bali kuendelea kushirikiana na zenye familia watoto wenye usonji.
“Niweke wazi kuwa mimi mwenyewe nina mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 16 yuko vizuri kimwili lakini hayuko vizuri kiufahamu huwa ninapoenda kushiriki matukio mbalimbali simwachi ninakwenda naye huwa anajisikia vizuri sana hasa leo naye ameshiriki mashindano na kujitwalia medali siwezi kumfungia ndani hata kutwa kutwa kwani nayeye ana haki kama wengine”amesema Bi.Hulda.
Hata hivyo amesema hii ni mbio za ni za kwanza na kufanyika hapa Nchi kwa kuwashirikisha watoto wenye usonji hivyo watendelea kufanya mara kwa Mara kwa kushirikiana na wadau wanaoguswa na jamii ya watoto wenye usonji kwa kuhamasisha jamii wachangamane na familia wenye watoto aina hiyo.