.

Waziri wa Kazi,Ajira,Sera,Bunge na watu wenye ulemavu Mh. Jenista Mhagama leo amezindua ripoti ya utafiti ya  Next Generation youth voices in Tanzania iliyofanywa na kwa malengo ya kutaka kujua  mitazamo ya vijana wa kitanzania.

Utafiti huo umefadhiliwa na Idara ya Uingereza ya maendeleo ya kimataifa(DFID)kwa lengo la kutaka kuangalia changamoto zinazo wakumba vijana,mitazamo na matarajio ya idadi  ya vijana Tanzania,pia kungalia vipaumbele vya vijana baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2015.

Aidha kwa upande wake Waziri Mhagama amewataka vijana kushiriki katika maamuzi yanayofanywa na na serikali ili kuepuka kuamuliwa mambo wasiyoyataka na kubaki wakilalamika mitaani bila hata ya ujumbe wao kufika sehemu husika’’Acheni kubweteka na kutaka kila kitu mfanyiwe,hangaikeni kutafuta taarifa zinazo wahusu ili muweze kujikwamua’’alisema Mh. mhagama.

Hata hivyo aliongeza kuwa serikali imejipanga kikamilifu kuwasaidia vijana kwa kuanzisha Saccos kila wilaya,hivyo vijana wanatakiwa kuunda vikundi ambavyo vitawawezesha kuweza kupata mikopo kirahisi kwani hata Mh rais ametenga milioni hamsini za kila kijiji kwaajiri ya maendeleo.

Kwa upande wake balozi wa uingereza hapa nchini bi, Dianna Melrose amesema kuwa vijana ndio taifa la kesho linalotegemewa kuja kuongoza nchi hivyo ni vyema kuwajengea mazingira mazuri ya sasa na baadae  ili kuandaa taifa lenye mwelekeo.

Utafiti huo unaonyesha kuwa vijana wengi wa kitanzania wanapenda tamaduni zao,amani,familia zao,dini,elimu ,afya,na hofu yao kubwa ni kutokuwa na uwezo wa kufikia ndoto zao  katika maisha,aidha ripoti hiyo imeonyesha asilimia (71%) ya vijana wana changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira na asilimia nne tu ndio waliokuwa na taarifa ya sera ya vijana na mpango wa uwezeshaji wa serikali kwa vjana.

TCU Yakanusha Taarifa za Kuvifungia Udahili wa Kozi Tofauti Vyuo 22
Diwani Ilala Atoa Wito Kwa Serikali na Mashirika Kusaidia Dar Festival