Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza sekta ya TEHAMA kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kazi nzuri wanayofanya ya kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali kidijitali
Waziri Mkuu amesema hayo katika Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA uliofanyika Arusha na kutoa rai ya kuongeza kasi katika kutengeneza miundombinu ambayo itachochea kufanyika kwa bunifu mbalimbali za kiteknolojia.
“Nipongeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kazi wanayofanya, Wizara ni changa kwa sababu tumeiunganisha lakini inafanya kazi nzuri ila nitoe rai kwa Wizara kuhakikisha bunifu zote zinazofanyika zinasimamiwa ili zitengeneze ajira kwa vijana wengi,”-amesema Waziri Mkuu, Majaliwa
Pia amesema kwa sasa teknolojia ndio inaendesha maisha kwa asilimia kubwa, hivyo amewataka wananchi kutumia teknolojia katika kutengeneza kipato