Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Saad Hariri ametangaza kujiuzlu baada ya kushindwa kuunda serikali kwa karibu miezi tisa.
Kwa mujibu wa Deutsche Welle, Hariri ametangaza uamuzi wake huo baada ya kukutana na Rais Michel Aoun ambapo amesema wameshindwa kufikia makubaliano.
Amesema kuwa Rais Aoun alikuwa ametaka marekebisho yafanyike kwenye safu ya mawaziri aliowapendekeza ameeleza kuwa wamejadili mambo yanayohusiana na uaminifu, na ni wazi kuwa hakuna chochote kilichobadilika.
Serikali ya Lebanon ilijiuzulu baada ya mlipuko mkubwa ambao ulitokea kwenye bandari ya Beirut mnamo Agosti 4 lakini imeendelea kufanya kazi katika hadhi ya serikali ya mpito.