Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameshangazwa na Shirikisho la soka nchini kumrudisha tena Kim Poulsen kuwa kocha mkuu wa timu ya vijana hapa nchini.

TFF kupitia kwa Rais wake Jamali Malinzi mapema mwaka huu alimtangaza kocha huyo kuwa kocha mkuu timu ya vijana nchini.

Waziri Majaliwa alishangazwa kusikia hivyo kuhoji ni TFF ilimrudisha kocha huyo ilihari walishamtimua kutokana na kuleta matokeo mabovu katika timu ya wakubwa ya Taifa Stars.

Na aliyasema hayo wakati alipokutana na vyama vya michezo mbalimbali hapa nchini siku ya jana kwa ajili ya kujua changamoto mbalimbali zinazosumbua katika vyama hivyo na zinazosababisha kushindwa kufanya vizuri kimataifa.

Mourinho Aendelea Kutoa Maelekezo Man Utd
John Terry Kubaki Magharibi Mwa London